Maafisa wa jeshi watangaza mapinduzi nchini Gabon

0
17

Maafisa wa Jeshi wamejitokeza katika televisheni ya Taifa nchini Gabon na kutangaza kutwaa mamlaka ya Taifa hilo.

Aidha, wametangaza kuwa wamebatilisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika juma lililopita ambapo Rais Ali Bongo alitangazwa kuwa mshindi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Bongo kuwa mshindi baada ya kupata mbili ya tatu ya kura kwenye uchaguzi huo ambao umekosolewa na upinzani kuwa ulighubikwa na udanganyifu.

Kupinduliwa kwa Rais Bongo kutapelekea ukomo wa utawala wa familia yake ambayo imeiongoza Gabon kwa miaka 53.

Wanajeshi hao mbali na kubatilisha matokeo, pia wamesitisha ufanyaji kazi wa taasisi zote za umma, kufunga mipaka ya nchi hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Rais Kagame aonya shughuli za kidini zinazotukuza umasikini

“Tumeamua kulinda amani kwa kuuondoa utawala uliokuwa madarakani,” ameeleza mmoja wa wanajeshi hapo kupitia kituo cha televisheni cha Gabon 24.

Mapinduzi hayo yameelezwa kuchochoewa na kutowajibika kwa Serikali, uongozi usiotabirika uliopelekea kuendelea kuwepo mmomonyoko wa kijamii ambavyo vingiweza kupelekea nchi kwenye machafuko.

Ali Bongo aliingia madarakani baada ya baba yake, Omar Bongo kufariki dunia mwaka 2009.

Mwaka 2019 kulikuwa na jaribio la mapinduzi, ambapo wanajeshi waliohusika walipelekwa gerezani.

Send this to a friend