Wananchi Gabon waunga mkono mapinduzi, Rais aomba msaada

0
25

Baada ya wanajeshi nchini Gabon kutwaa mamlaka ya nchi hiyo wakibatilisha matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais Ali Bongo, Rais Bongo ameonekana kwenye kipande cha video akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa duniani kupaza sauti zao kuhusu mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Akiwa ameketi katika eneo ambalo amedai ni makazi yake, Bongo amesema ametenganishwa na familia yake na hajui walipo mpaka sasa. “Hakuna chochote ninachojua kinaendelea. Sijui kinachotokea,” amesema.

Sababu za kuondolewa kwa Rais Bongo zimetajwa kuwa ni uchaguzi uliojaa udanganyifu na uliopata ukosoaji mkubwa. Inaelezwa kuwa waangalizi wa kimataifa na waandishi wa habari walizuiliwa kufuatilia au kuripoti kuhusu uchaguzi huo.

Wajue Marais wa Afrika waliopinduliwa na jeshi wakiwa madarakani 

Hata hivyo, baada ya kumiliki madaraka tangu mwaka 19, wengi wanahisi kuwa familia ya Bongo imetawala kwa muda mrefu sana, hii imepelekea watu kujitokeza mitaani kuonyesha furaha yao wakionekana kuwa kweli wamefurahia hatua iliyochukuliwa.

Ufaransa ambayo imekuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika kwa muda mrefu, imetoa taarifa za kulaani tukio hilo. Hata hivyo ushawishi wa Ufaransa barani Afrika umepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, na wito wa kuendelea kwa utawala wa Ali Bongo huenda ukaendelea kukakataliwa na wananchi wa Gabon.

Send this to a friend