Majibu ya Katiba kuhusu uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu

0
24

Rais Samia Suluhu Hassan Agosti 30 mwaka huu amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, moja ya mabadiliko makubwa aliyoyafanya ni pamoja na kumhamisha aliyekuwa Waziri wa Madini, Dotto Biteko kuwa Waziri wa Nishati na pia kumteua kuwa Naibu Waziri Mkuu jambo ambalo limezua hoja nyingi juu ya cheo hicho.

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hakuna kifungu kinachozungumzia moja kwa moja kuhusu cheo cha Naibu Waziri Mkuu, lakini Ibara ya 36 (1) Katiba hiyo inampa Rais mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya umma.

Rais Samia afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Katibu na Naibu Makatibu

“Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”

Biteko anakuwa kiongozi wa tatu katika historia ya Tanzania kushika wadhifa huo baada ya Dkt. Salim Ahmed Salim na Augustino Mrema.