TPA yatangaza fursa ya uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam

0
17

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imealika kampuni kutuma zabuni kwa ajili ya kusimamia kituo cha makontena (Container Terminal II) kinachohusisha gati namba 8 hadi 11 katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hii ni eneo ambalo hapo awali lilisimamiwa na kampuni binafsi ya kimataifa ya kuhudumia makontena Tanzania (TICTS) kwa miaka 22, kampuni inayomilikiwa kwa kiasi kikubwa na Hutchison Ports ya Hong Kong.

Tanzania pia kwa sasa inaendeleza mazungumzo na DP World, kampuni kubwa ya huduma za bandari ya Dubai, ili kusimamia gati namba moja hadi hadi saba katika bandari hiyo.

Tanzania inaboresha miundombinu kwenye Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi utakaoiwezesha kushindana na bandari nyingine, ikiwemo bandari ya Mombasa nchini Kenya.

Kama sehemu ya mipango ya Tanzania, DP World itasimamia magati 1-7, huku mwendeshaji mwingine wa kimataifa wa bandari akiendesha gati namba 8-11 kwa lengo la kuleta ufanisi wa hali ya juu.

Send this to a friend