Nchi 10 za Afrika zenye uwekezaji mkubwa kutoka nje

0
24

Uwekezaji ni mchakato wa kutumia rasilimali au fedha katika miradi au biashara kwa matumaini ya kupata faida au kurudisha uwekezaji huo. Katika ngazi ya kimataifa, uwekezaji huchukua sura ya Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) ambapo wawekezaji kutoka nje ya nchi wanawekeza katika miradi ndani ya nchi nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo (UNCTAD) 5 Julai 2023, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) kwa mwaka 2022 imepungua sana barani Afrika ambao ulikusudiwa kwa bara hilo linaloinuka kiuchumi.

Nchi 10 za Afrika zenye intaneti yenye kasi zaidi

Kulingana na ripoti hiyo, kiasi cha pesa ambacho wawekezaji wa kimataifa walipeleka Afrika kilishuka sana kutoka dola bilioni 80 mwaka 2021 hadi dola bilioni 45 mwaka 2022.

Hii ni orodha ya nchi 10 za Afrika zenye uwekezaji mkubwa wa kigeni, pamoja na thamani ya uwekezaji (TZS) kulingana na nchi zilizotajwa kwenye ripoti;

1. Misri: Trilioni 27.6
2. Afrika Kusini: Trilioni 22.5
3. Ethiopia: Trilioni 9.3
4. Senegal: Trilioni 6.5
5. Morocco: Trilioni 5.3
6. DR Congo: Trilioni 4.5
7. Ghana: Trilioni 3.8
8. Uganda: Trilioni 3.8
9. Tanzania: Trilioni 2.8
10. Zambia: Bilioni 290.6

Chanzo; Business Insider

Send this to a friend