Mtu mmoja amekamatwa nchini Rwanda baada ya zaidi ya miili ya watu 10 kugunduliwa ikiwa imezikwa katika shimo lililokuwa limechimbwa ndani ya jiko la nyumba yake mjini Kigali nchini Rwanda.
Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 34 anayeshukiwa kuwa muuaji, na inasemekana aliwachukua wahanga kutoka katika baa na kuwaleta hadi nyumbani kwake ambapo amepanga katika eneo la kitongoji cha Kigali.
Inaelezwa kuwa mshukiwa huyo awali alikamatwa mwezi Julai kwa tuhuma za wizi na ubakaji pamoja na makosa mengine, lakini alipewa dhamana kutokana na ukosefu wa ushahidi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.
JWTZ: Tunaingia mtaani kuzisaka sare zetu kwa wananchi
Chanzo cha RIB kimeeleza kuwa “mshukiwa alikiri kwamba alijifunza kuua kwa kuchunguza wauaji maarufu wa kihistoria na kwamba aliwasha acid ili kuyeyusha baadhi ya miili ya wahanga wake.”
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mtuhumiwa huwalenga wale wasiokuwa na familia au marafiki wa karibu au wanaofanya biashara ya ngono na kuwapeleka nyumbani kwake kisha huwanyang’anya simu zao na mali na kuwakandamiza hadi kufa, na kisha huwazika katika shimo.