Kwanini India inakusudia kubadili jina lake?

0
59

Mjadala mkubwa umeibuka nchini India baada ya Serikali ya Waziri Mkuu, Narendra Modi kuitaja nchi hiyo kama Bharat kwenye mialiko rasmi ya mkutano wa G20, na kuwaacha wengi wakijiuliza ikiwa jina hilo litabadilishwa au la.

India inakusudia kubadili jina na kutambulika kama ‘Bharat,’ ambapo pendekezo hilo litawasilishwa katika mkutano maalumu wa bunge utakaoketi kuanzia Septemba 18-22 mwaka huu.

Rais wa India, Droupadi Murmu alilitumia jina hilo kwenye mialiko wa chakula maalum kwa ajili ya mapokezi aliyokuwa akiandaa kwa viongozi katika mkutano wa G20 jijini New Delhi, akijitambulisha kama ‘Rais wa Bharat’.

Ikiwa hufahamu, India pia inaitwa Bharat, au Bharata, au Hindustan. Hayo yote ni majina yake kabla ya ukoloni katika lugha za India.

Kwanini mabadiliko haya yanatokea?

Chama tawala cha kitaifa cha Bharatiya Janata Party, au BJP cha Waziri Mkuu Narendra Modi kimekuwa kikibadilisha majina yaliyotolewa na wakoloni, wakisema kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia India kuondokana na mawazo ya utumwa wa kikoloni.

Wafuasi wa mabadiliko ya jina hilo wanadai kwamba wakoloni wa Uingereza ndio walioanzisha jina ‘India’ wakati jina halisi lilikuwa Bharat.

Baadhi ya wanasiasa wanapinga uamuzi huo na wengine wakidai kuwa Serikali haikuwa na haja ya kubadili jina hilo kwakuwa jina la nchi, yaani ‘India,’ limejijengea umaarufu na hadhi thabiti kwa karne nyingi katika historia ya nchi hiyo.

Send this to a friend