Serikali Kenya yapunguza gharama ya umeme

0
29

Kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wateja nchini Kenya kuhusu bei ghali ya umeme, sasa Wakenya wanafurahia kupunguzwa kwa bei ya tokeni za umeme baada ya Kenya Power kuanzisha punguzo la bei.

Uchunguzi uliofanywa na Kenyans.co.ke umeeleza kuwa kwa KSH 1,000 [TZS 17,114] watumiaji wanapokea uniti 37.61 katika mwezi wa Septemba, ikilinganishwa na uniti 31.15 tu katika mwezi wa Agosti.

Kwa upande mwingine, wale wanaotumia KSH 100 [TZS 1,700] wanapata uniti 3.76 ya umeme mwezi Septemba, ikilinganishwa na 3.67 katika mwezi wa Agosti, na 3.59 mwezi Julai.

Taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kenya Power, Joseph Siror, zimebainisha kuwa umeme sasa ni chanzo cha nishati chenye bei nafuu zaidi nchini humo.

Kenya Power ilikanusha ripoti za vyombo vya habari mnamo Agosti 8, ambazo zilidai kuwa walikuwa wakiongeza bili za umeme kwa asilimia 20 na kusisitiza kuwa ripoti hizo zilikuwa zikilenga kujenga taswira potofu kuhusu gharama ya umeme na kudhalilisha sifa ya kampuni.

Send this to a friend