Watu 10,000 wahofiwa kupotea kutokana na mafuriko nchini Libya

0
19

Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu (IFRC) limebainisha kwamba takriban watu 10,000 wanahofiwa kupotea kutokana na mafuriko makubwa nchini Libya.

Zaidi ya miili 1,000 tayari imepatikana katika mji wa Derna pekee, na maafisa wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka baada ya Dhoruba Daniel kuvuma katika Bahari ya Mediterranean na kuingia nchini humo.

“Tunaweza kuthibitisha kutoka kwa vyanzo vyetu huru vya habari kwamba idadi ya watu waliopotea inafikia 10,000 hadi sasa,” alisema Tamer Ramadan, mkuu wa ujumbe wa IFRC nchini Libya.

Mafuriko haya na maporomoko ya udongo yanayosababishwa na mvua kubwa yameharibu barabara na nyumba nyingi. Eneo lililoathirika zaidi ni bandari ya Derna, ambapo sehemu kubwa ya eneo hilo iko chini ya maji baada ya mabwawa mawili na madaraja manne kuporomoka.

Send this to a friend