Mambo 8 ya kuzingatia unapoomba leseni ya udereva kwa mara ya kwanza

0
45

Kuomba leseni ya udereva kwa mara ya kwanza ni hatua muhimu katika kuanza safari yako ya kuwa dereva. Kama unahitaji kuendesha chombo cha moto barabarani, unahitaji kuwa na leseni itakayokupa kibali na kukuepusha na kukamatwa na afisa wa usalama barabarani.

Ikiwa ni mara ya kwanza unaomba leseni haya ni mambo ya kufuata;

1. Uwe umehudhuria mafunzo katika chuo chochote kinachofahamika na kupewa cheti.

2. Uwe na umri wa miaka 18 au zaidi kwa ajili ya gari na umri wa miaka 16 na kuendelea kwa ajili ya pikipiki.

3. Uwe na leseni ya kujifunzia/ya muda ya udereva.

4. Uwe umelipa ada ya kufanyiwa majaribio – GRR.

5. Uwe na cheti cha kupimwa macho.

6. Uwe umepeleka maombi kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.

7. Uwe umekwenda ofisi ya polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.

8. Baada ya mwombaji kufanyiwa majaribio anaweza kuruhusiwa kuendesha pikipiki na magari madogo.

Send this to a friend