Rais Samia: Kukatika kwa umeme si tatizo la mtu, ni la kitaifa

0
14

Kutokana na changamoto iliyopo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amempa miezi sita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Gissima Nyamo-Hanga kuhakikisha anatibu tatizo hilo.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 26, 2023 wakati akiwaapisha viongozi wateule Ikulu jijini Dar es Salaam, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.

“Nyamo-Hanga unakwenda TANESCO nikijua kwamba wewe unaijua vizuri TANESCO, kwa hiyo utakwenda pale kuongeza pale Maharage alipofikia. Tuna crisis [changamoto] crisis ile ni crisis yetu kama taifa si ya mtu,” amesema.

Ameongeza kuwa “tatizo la kukatika katika kwa umeme si la mtu, ni letu kitaifa. Kwa hiyo sasa tumejipanga vizuri tunafanya ukarabati wa hizo mashine lakini pia tuna mipango mingine ya kujenga ma-substation [vituo vya kupoza umeme] na mengineyo kuunganisha mikoa kwenye gridi ili umeme usikatike.”

Aidha, amesema amefanya uamuzi wa kumwoindoa Maharage Chande TTCL ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na kumhamishia Shirika la Posta Tanzania kama Postamasta Mkuu kutokana na ubobezi alionao kwenye sekta hiyo.

Send this to a friend