Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetangaza kukamilisha utaratibu wa uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kufikia Oktoba 31, mwaka huu kwa zaidi ya TZS bilioni 501.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema mradi huo uliosimama ujenzi kwa takriban miaka saba umeuzwa kama ulivyo ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama ambazo ziliwekezwa hapo awali.
Kwa mujibu wa NSSF, mpaka kufikia uamuzi wa kuuzwa kwa mradi huo, tayari umetumia zaidi ya TZS bilioni 330.
Padri aliyetuhumiwa kubaka mtoto wa miaka 12 ashinda kesi
“Kwa sasa mfuko kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali unakamilisha taratibu za zabuni baada ya kukamilika kwa hatua ya tathmini ya zabuni na maafikiano ya bei. Maturation ni kusainiwa kwa mkataba wa mauzo ya mradi huu kabla ya Oktoba 31, 2023,” amesema.
Mshomba amesema wanaamini kuwa mnunuzi ataendelea na mpango huo kama ilivyokuwa imekusudiwa.