Tanzania kuuza sukari nje ya nchi miaka miwili ijayo

0
24

Serikali imesema Tanzania inatazamiwa kuanza kuuza sukari nje ya nchi ndani ya miaka miwili ijayo kutokana na jitihada mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na viwanda vya ndani.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdalah wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Kagera kwa lengo la kuangalia uzalishaji unaoendelea kiwandani hapo akiambatana na viongozi mbalimbali.

“Ile ndoto ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kuilisha Afrika na dunia kwa ujumla, sasa inaanza kutafsirika kwa vitendo. Na suala la kuagiza sukari nje ya nchi, sasa linaenda kufikia kikomo. Tutailisha Afrika na dunia kupitia kiwanda cha Kagera Sugar,” amesema.

TPA yatangaza fursa ya uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam

Aidha, amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kujenga viwanda vingi vya sukari nchini ili Tanzania iweze kujitosheleza na kuacha kuagiza sukari nje ya nchi.

Send this to a friend