Utafiti: Wasichana wengi walioachwa na wachumba zao hupata ukichaa

0
32

Idadi ya wasichana wanaochumbiwa na kuvishwa pete kisha kuachwa na wanaume zao imezidi kuongezeka na kuwapelekea wengi wao kupata kichaa na msongo wa mawazo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo wa Mwanamke Shujaa iliyopo mkoani Morogoro, Dkt. Magdalena Kongera wakati wa tamasha la kupinga ukatili wa kijinsia ambapo amebainisha kuwa asilimia 10 kati ya wasichana 100 ambao hukataliwa na wanaume hao, hupatwa na kichaa kutokana na msongo wa mawazo unaosababishwa na maumivu ya kukataliwa.

Amesema wasichana wanaokataliwa hupatwa na tatizo la kisaikolojia linalojulikana kitaalamu kama “divorce psychosis” na pia hupoteza uwezo wa kujiamini, hamu ya kula na hujihisi kuwa hawafai mbele ya jamii, kujiona hawana mvuto pamoja na kuppoteza imani kwa wanaume wengine.

Dar yaongoza kwa idadi ya wanaong’atwa na mbwa

“Wasichana hawa huchanganyikiwa akili na kujikuta katika hali ya kujikataa huku wengine hufikia uamuzi wa kutaka kujiua,” amesema.

Send this to a friend