Hospitali ya Temeke yaondoa viungo vya uzazi vya kike kwa mgonjwa mwenye jinsia mbili

0
14

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imefanya upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye mwonekano wa jinsia ya kiume ikiwa ni mara ya kwanza upasuaji huo kufanyika katika hospitali hiyo na kwa hospitali za rufaa zilizopo Tanzania.

Upasuaji huo umefaywa na jopo la madaktari kutoka hospitali hiyo, na limeongozwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Jumla na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Hussein Msuma pamoja na wasaidizi wake. Dkt. Hamis Mbarouk, Curtius Mbalamula, Mkati na Shani Maupa.

Taarifa ya hospitali hiyo imeeleza kuwa kufanyika kwa upasuaji huo ni moja ya mafanikio makubwa katika sekta ya afya Tanzania kwa kuwa moja ya jitihada ya serikali na wizara ya afya kwa ujumla ni kuhakikisha hospitali zina uwezo wa kutoa matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi.

Dar yaongozwa kwa wanaong’atwa na mbwa

Akizungumza baada ya upasuaji kufanyika na kufanya vipimo vya sampuli zilizo tolewa katika upasuaji, Dkt. Msuma amesema mgonjwa alifika hospitalini akiwa na mwonekano wa jinsia ya kiume lakini ana maumbile ya ndani ya aina mbili, yaani umbile la kike na la kiume, hivyo kupelekea upasuaji huu.

“… alikuwa na mifumo ya uzazi ya jinsia mbili, ya kiume kwenye korodani ya kulia na ya kike kwenye korodani ya kushoto,” amesema.

Ameongeza hali hiyo inatokana na changamoto ya ukuaji wa kijinsia (ovotesticular DSD), ni kwamba ni nadra na adimu sana kutokea ambapo binaadamu huzaliwa na viungo vya ndani vya uzazi (gonadi) za jinsia zote (ovari za kike na korodani za kiume).

Send this to a friend