EQUITY BANK YAZINDUA HUDUMA YA KIDIJITALI ‘LIVE CHAT’
Benki ya Equity imezindua huduma ya Kidigital ya Light Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 4, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Equity Bi. Isabella Maganga, amesema katika kuanzimisha wiki ya huduma kwa wateja wamezindua huduma ya Light Chat ili kuwafikia wateja na kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora na rafiki.
“Huduma hii inakwenda kutuweka karibu na wateja wetu ambapo mteja na mtoa huduma wanaongea moja kwa moja live kutoa huduma papo kwa papo” amesema Bi. Maganga.
Bi. Maganga amesema kazi yao kubwa ni kutoa huduma ya fedha na kuendelea kujituma na kubuni huduma zao, huku akieleza kuwa watahakikisha wateja wao wanaendelea kufurahia huduma zao za kibenki.
Pamoja na hayo amesema Kituo cha huduma kwa wateja wanazidi kukipanua na kuongeza huduma zaidi ili waendelee kuwa karibu zaidi na wateja wao na kuendelea kutoa huduma kwa muda wote asubuhi mpaka usiku.
“Nawakaribisha sana wateja wetu Equity na pia nawashurku kwa kutuamini sisi ambao tunawapa huduma za kibenki na pale tunapokua tunatimiza malengo yao ya shughuli zao za kiuchumi na kijamii”
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya EQUITY, Isabela Maganga akizindua huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima. Huduma hiyo imeiznduliwa leo Oktoba 4,2023 katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Equity Tawi la Mwenge, Magreth Makundi ameahidi kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa kiwango Cha juu kabisa na kuwaahidi wateja wao wote na kuendelea kupata huduma bora zaidi.
Aidha amewashukuru wateja kwa kusherekea pamoja katika muda wote wa wiki ya huduma kwa wateja, huku akiahidi kuendelea kufanya vizuri katika sekta ya Benki.
Naye Magreth Makundi Meneja wa Tawi la Mwenge Benki ya Equity, amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa kiwango cha juu.
Amesema kuwa huduma ya Kidigital ya Light Chat inakwenda kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa kuwa karibu na wateja wao katika kutoa huduma.
Watumishi wa Benki ya Equity wakiwa kwenye picha ya pamoja wa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima. Huduma hiyo imeiznduliwa leo Oktoba 4,2023 katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.