Wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili waongezeka kwa kasi

0
26

Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Mwananyamala imeripoti ongezeko la wagonjwa wa matatizo ya afya ya akili kutoka wastani wa watu watano hadi nane awali mpaka kufikia wastani wa 30 hadi 45 kwa siku.

Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Zavery Benela wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika Wiki ya Afya ya Akili ambapo amesema ongezeko hilo la wagonjwa linatokana na visababishi mbalimbali vikiwemo vya kibaiolojia, kisaikolojia na kimazingira jambo ambalo amesema linahitaji wataalamu ili kulidhibiti.

Hizi ndizo fani 6 zitakazopewa mikopo kwa wanafunzi wa Diploma

“Kuanzia Juni mwaka jana, tumeanza kupata ongezeko kubwa la wagonjwa wa aya ya akili ambalo linafikia wagonjwa 30 mpaka 45 kwa siku. Kabla tulikuwa tunapata wagonjwa watano mpaka wanane kwa siku, jambo linaloonesha uhitaji wa kuwapo wataalamu wa magonjwa ya afya ya akili katika hospitali zetu,” ameeleza.

Kutokana na ongezeko hilo, Dkt. Benela ametoa wito kwa wataalamu wa fani za udaktari kusoma pia udaktari wa afya ya akili kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa wataalam hao kwa sasa.

Send this to a friend