Rais Samia: India ni mshirika na mwekezaji mkubwa wa Tanzania

0
15

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na India zinalenga kuimarisha ushirikiano zaidi wa kimkakati hasa katika biashara na uwekezaji utakaosaidia nchi hizo mbili kusonga mbele kimaendeleo.

Rais ameyasema hayo alipokuwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi katika mazungumzo na waandishi wa habari mara baada ya sherehe ya mapokezi jijini New Delhi nchini humo kwa ajili ya ziara ya siku nne.

“Kufikia mwaka 2022, takwimu zinaonyesha kwamba India ilifanya uwekezaji wa Dola za Marekani bilioni 3.1 [TZS trilioni 7.8] nchini Tanzania. Hii inafanya India kuwa mshirika wa tatu kwa ukubwa katika biashara na mwekezaji wa tano kwa ukubwa katika nchi yetu. Hii ni ishara nzuri ya uhusiano wa kibiashara na uwekezaji ulioimarika kati ya nchi zetu mbili,” amesema.

Rais Samia ameongeza kuwa “tulipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na serikali ya India. Katika mazungumzo hayo, niliweza kuona jinsi serikali ya India ilivyo na hamu na azma ya kuimarisha na kukuza uhusiano wetu.”

Waziri Mkuu abaini viongozi wanatoa zabuni kwa kampuni zao kupima ardhi

Aidha, amepongeza na kushuruku mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya India kwa miongo kadhaa katika uchumi wa Tanzania huku akiamini kuwa uhusiano huo utaendelea kudumishwa ikiwa ni mategemeo ya waasisi wa mataifa hayo mawili Mwalimu Julius Nyerere na Mahatma Gandhi.

Send this to a friend