Ukuaji wa uchumi ni mchakato unaotokea katika uchumi wa nchi au eneo ambapo uzalishaji wa bidhaa na huduma unakuwa kwa kasi na kusababisha ongezeko la thamani ya uchumi.
Ukuaji huu wa uchumi unaweza kuonyeshwa kupitia viashiria kama vile Pato la Taifa, ajira, na ongezeko la mapato ya watu.
Kuna sababu kadhaa zinazochangia ukuaji wa uchumi, ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa ndani na nje, maendeleo ya teknolojia, kuongezeka kwa uzalishaji wa sekta muhimu kama viwanda na huduma, na mazingira mazuri ya biashara. Ukuaji wa uchumi husaidia kupunguza umaskini, kuongeza fursa za ajira, na kuboresha maisha ya watu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya Septemba ya Africa Pulse, shughuli za kiuchumi katika Kusini mwa Jangwa la Sahari (SSA) zinatabiriwa kupungua zaidi kutoka asilimia 3.6 mwaka 2022 hadi asilimia 2.5 mwaka 2023, ambayo ni marekebisho ya chini ya asilimia 0.6 kutoka utabiri uliokuwemo katika toleo la Aprili 2023 la ripoti hiyo.
1. Rwanda: 5%-6%
2. DR Congo: 5%-6%
3. Côte d’Ivoire: 5%-6%
4. Mozambique: 5%-6%
5 Ethiopia: 4%-6%
6. Benin: 4%-6%
7. Cabo Verde: 4%-6%
8. Uganda: 3% -5.5%
9. Togo: 3%-5%
10. Tanzania: 3%-5%