Rais Samia: Tumeanza kazi ya kuisuka upya Wizara ya Mambo ya Nje

0
21

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameunda tume ya Kutathmini Ufanisi na Utendaji Kazi Wizara ya Mambo ya Nje ili kuirudishia hadhi yake na kuipa umahiri kwa kuwa hali iliyokuwa ikiendelea wizarani humo ilisababisha wizara hiyo kudorora na baadhi ya maeneo yake kukwama kiutendaji.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya Kamati Kutathmini Ufanisi na Utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, amesema panga pangua za watumishi waandamizi ndani ya wizara hiyo imepelekea wizara hiyo kuwa na utendaji usioridhisha na kupwaya.

“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka taasisi za kimataifa zilizopo nchini kuhusu utendaji usioridhisha wa wizara hii. Hapo ndipo niliapoamua na kuona ulazima wa kuifanyia tathmini na kuirudishia hadhi yake ili kuwe na umahiri ule ambao tunautarajia,” amesema.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini Ufanisi na Utendaji kazi Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Hassan Yahya katika ripoti hiyo kwa niaba ya kamati, amependekeza jina la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki libadilishwe na badala yake liwe ‘Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa ili kuakisi azma ya serikali ya kutumia diplomasia ya uchumi katika kujenga ushirikiano wa kimataifa.

Send this to a friend