Rais Samia: Serikali inawekeza nguvu kubwa kwa vijana

0
13

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeweka jitihada kubwa katika kuwawezesha vijana kutumia rasilimali za nchi zilizopo ili kujiletea maendeleo na kuboresha maisha yao.

Akizungumza katika Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Manyara, Rais Samia amesema Serikali inaweka nguvu kubwa katika maeneo ya utalii, madini, viwanda vidogo, kilimo biashara, michezo, sanaa na ubunifu pamoja na kujenga vyuo vya ufundi nchi nzima ili viwezeshe ajira kwa vijana.

“Tunataka kila wilaya iwe na chuo cha VETA. Tunataka vijana wapate ujuzi utakaowawezesha kuingia kwenye shughuli za ujasiriamali pamoja na uzalishaji wa bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kama ilivyobainishwa katika programu yetu ya Jenga Kesho Bora (BBT),” amesema.

Ameongeza, “endapo tutakuwa na vijana wazembe, wavivu, wazururaji wasiowajibika wala kujitambua, vijana hawa watakuwa mzigo mkubwa kwa nchi yetu.”

Aidha, amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kote nchini kusimamia kikamilifu ili kuhakikisha kilimo cha bangi na dawa za kulevya zinakomeshwa katika mikoa yao ili kuokoa kizazi cha vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.

Mikoa 12 yenye kiwango kikubwa cha udumavu Tanzania

Mbali na hayo amewataka watumishi wa umma kuzingatia nidhamu na kuachana na matumizi ya lugha chafu kwa wananchi, kuchelewesha utoaji huduma na rushwa.

Send this to a friend