Gari dogo, lori vyagongana na kuua watatu Pwani

0
16

Watu watatu wamefariki na wengine wanne wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha gari dogo kugongana uso kwa uso na lori katika Kijiji cha Mbala Vigwaza mkoani Pwani usiku wa Oktoba 23, 2023.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2023 Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendokasi wa dereva wa gari dogo aina ya Toyota Kluger lililokuwa likitokea mkoani Iringa kuelekea jijini Dar es Salaam.

“Waliokuwa kwenye gari dogo walikuwa wanatoka Iringa kuelekea Dar es Salaam na huyu wa lori aina ya Scania alikuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro, lakini dereva wa gari dogo alikuwa na mwendo mkali bila kuchukua tahadhari,” amesema.

Aidha, amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Mbuma anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (35-40), Pokera (19) wote wakazi wa Mbezi, Dar es Salaam na Mwanahamisi (18) mkazi wa Kijitonyama mkoani Dar es Salaam.

Send this to a friend