Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema hali ya upatikanaji wa mafuta nchini ni ya kuridhisha kutokana na hatua zinazochukuliwa na mamlaka hiyo kudhibiti ufichaji wa mafuta.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari jiijni Dar es Salaam ambapo amesema changamoto ya upungufu wa mafuta nchini ilichangiwa na baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta kuhodhi ili kujipatia faida kubwa kinyume na sheria.
“EWURA iliendelea na uchunguzi wa vituo vingine zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa ya kuwasilisha utetezi wao. Baada ya kupitia utetezi wao EWURA imejiridhisha pasipo shaka kuwa vituo vingine viwili vilitenda kosa la kuhodhi mafuta kati ya mwezi Julai na Agosti 2023, na hivyo tutavifungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Oktoba 26, 2023,” ameeleza.
Matajiri 10 wakongwe zaidi Afrika
Aidha, EWURA imetoa onyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kuwa serikali inafuatilia suala hilo kwa ukaribu kupitia vyombo vyake mbalimbali, na kwamba endapo itathibitika kuna uvunjaji wa sheria na kanuni, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuwafutia leseni zao.