Wanaotengeneza biskuti zenye bangi wakamatwa Dar es Salaam

0
57

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata kilogramu 423.54 za bangi iliyosindikwa, maarufu kama skanka, katika operesheni maalum zilizofanyika kwenye mipaka na fukwe za Bahari ya Hindi.

Aidha, mamlaka imewakamata watu 16 wanaojihusisha na utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na skanka (bangi yenye kiwango kikubwa cha sumu) katika eneo la Kawe, Dar es Salaam, ambapo watuhumiwa walikutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengeneza biskuti za bangi.

Kati ya watuhumiwa hao, 10 wamefikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Jeshi la Polisi lawashikilia watu saba kwa kumteka mwanamke Masaki

Taarifa hiyo imefafanua kuwa bangi aina ya skanka hutokana na kilimo cha bangi mseto ambapo asilimia 75 ni bangi aina ya sative na asilimia 25 ni bangi aina ya indica.

Kiwango cha sumu kilichopo kwenye skanka ni zaidi ya asilimia 25 ukilinganisha na bangi ya kawaida ambayo kiwango chake cha sumu ni kati ya asilimia 3 mpaka 10 na hivyo madhara yake ni makubwa zaidi ikiwemo kuamsha na kuzidisha magonjwa ya afya ya akili kwa haraka.

Send this to a friend