Sheikh Ponda na wenzake tisa wakamatwa wakitaka kuandamana

0
23

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 10 akiwemo kiongozi wa maandamano, Sheikh Ponda ambao walijitokeza katika viwanja wa Mnazi Mmoja kwa ajili ya kufanya maandamano hadi Manzese, Dar es Salaam kama ilivyopangwa.

Akizungumza na Swahili Times, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema jeshi linawashikilia wanawake wanne na wanaume sita waliojitokeza leo ambapo hadi sasa hawajajua lengo kuu la mkusanyiko huo.

“Baada ya kufika sisi tulimzuia na tuko naye tunafanya naye mahojiano. Wamefika pale wakawa hawajafanya lolote nadhani walikuwa wanataka kuongea na nyinyi waandishi wa habari, lakini hatukujua mkusanyiko ulikuwa wa nini, kwa sababu alikuwa amekwisha hamasisha, sisi tumepata fursa ya kumchukua na kumhoji,” amesema

Miaka 8 jela kwa kumuua mchepuko wa mumewe

Kamanda Muliro amesema baada ya mahojiano na watu hao taratibu zingine zitafuatwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zimeeleza kuwa dhumuni ya maandamano hayo ilikuwa ni kutetea mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazi Mmoja hadi Manzese.

Send this to a friend