Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema wananchi walio tayari kupokea fedha zao za fidia ili kupisha utekelezaji wa mradi wa uendelezwaji wa eneo la bonde la mto Msimbazi walipwe mara moja.
Amesema hayo Novemba 15, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa maeneo ya Jangwani, Mchikichini na Magomeni Suna wanaoathirika na mafuriko ya Jangwani katika mto Msimbazi.
Biteko aiagiza REA kuachana na wakandarasi wazembe
“Pamoja na kwamba sheria haiwatambui wananchi waliojenga Jangwani kwa kuwa hawapo kisheria ila Rais Samia Suluhu Hassan ameonelea kuwapa kifuta jasho. Ni fidia ya shilingi milioni nne kwa takribani wananchi 2400 katika asilimia 92 ya wananchi walioridhia,” amesema Mchengerwa.
Chanzo: Habari Leo