Bibi harusi aliyefariki ajalini kuzikwa siku ya harusi

0
14

Aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa, Rehema Chao (37) ambaye amefariki kwenye ajali pamoja na mama yake mzazi wakitoka kwenye ‘send off’ wanatarajiwa kuzikwa Desemba 02, 2023 nyumbani kwao kijiji cha Nganyeni, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro siku ambayo ilipangwa kwa ajili ya harusi.

Ajali hiyo ilitokea Jumatano Novemba 29 mwaka huu baada ya gari walilokuwa wamepanda, aina ya Toyota Raum, kugongana na roli wakati Rehema aliyekuwa akiendesha alipojaribu kulikwepa shimo na kukutana na lori eneo la Kichwa cha Ng’ombe wilayani humo.

Rehema ambaye alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Sua mkoani Morogoro baada ya send off yake kuisha alianza safari ya kuelekea nyumbani kwao Marangu akiwa ameambatana na familia yake kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake ambayo ingefanyika mkoani Arusha.

Hata hivyo Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema wanamshikilia dereva wa lori, Joachim Meela (37) kwa ajili ya mahojiano zaidi huku majeruhi, Veronika Chao (35) ambaye ni mdogo wa marehemu na mwanaye Jayden Erasto (2) wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Send this to a friend