Nchi 10 zilizopeleka wajumbe wengi zaidi COP28 (Dubai)

0
21

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP) hufanyika kila mwaka kujadili masuala yanayohusu mabadiliko ya tabianchi. Mkutano huu hufanyika chini ya mwamvuli wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) na unajumuisha serikali, wawakilishi wa kibiashara, mashirika ya kiraia, wanasayansi, na wadau wengine kutoka kote duniani.

Kwa mwaka huu katika COP28, zaidi ya wakuu wa nchi 140, wawakilishi wa Serikali, wajumbe na washiriki takribani 70,000 wamekusanyika katika Jiji la Expo Dubai, UAE kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 12, 2023, ambapo udhibiti wa nishati ya mafuta na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu ni kati ya ajenda za mkutano huo.

Nchi mbalimbali zinazoshiriki mkutano huo zimewasilisha wajumbe mbalimbali wakiwemo maafisa wa serikali, wataalamu wa mazingira, wanasayansi, wawakilishi wa mashirika binafsi, na viongozi wa kisiasa ambapo kwa Afrika Nigeria imetajwa kupeleka wajumbe wengi zaidi.

Hii ni orodha ya nchi 10 zilizopeleka wajumbe wengi zaidi katika mkutano huo;

  1. Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE): 4,409
  2. Brazil: 3,081
  3. Nigeria: 1,411
  4. China: 1,411
  5. Indonesia: 1,229
  6. Japan: 1,067
  7. Uturuki: 1,045
  8. India: 948
  9. Morocco: 823
  10. Ufaransa: 800

Tanzania imewakilishwa na wajumbe 763 waliojiandikisha kuhudhuria mkutano huo, ambapo kati yao, asilimia 48.6 wametoka sekta binafsi.

Send this to a friend