Katibu Mkuu CWT aliyegoma kurudi kufundisha asimamishwa kazi

0
16

Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika mkoani Dar es Salaam, Maganga Japhet kutokana na tuhuma za utoro kazini.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza kuwa sababu za kusimamishwa kazi kwa mwalimu huyo ni pamoja na kutotii maelekezo ya viongozi wake.

Mkenya aajiriwa kwenye nafasi za juu za mashirika 8 ya umma

Maganga alichaguliwa Desemba 2022 na Mkutano Mkuu wa CWT kuwa Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Deus Seif, ambapo awali alikwa akitumikia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu. Januari 25 mwaka huu Maganga, Makamu wa Rais wa CWT, Dinna Mathaman na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Wakuu wa Wilaya lakini Maganga na Mathaman hawakufika kuapa.

Aidha, mwalimu huyo aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT kwa mara ya tatu mara baada ya muda wake kumalizika Septemba 30, mwaka huu ambapo Katibu Mkuu UTUMISHI hakuridhia maombi hayo na kumtaka kurejea kwenye kituo chake cha kazi Temeke.

Send this to a friend