Dawa za uchungu za mitishamba zinavyoongeza vifo vya wajawazito

0
15

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachuzibwa ameseama matumizi ya dawa za mitishamba kwa ajili ya kuongeza uchungu kwa akina mama wajawazito wanaolazwa katika hospitali na vituo vya afya mkoani humo imekuwa ni moja ya sababu ya vifo vya akina mama.

Amesema baada viongozi na wataalam wa afya kugundua uwepo wa hali hiyo, walifanya udhibiti kuanzia pindi mama mjamzito anapokuwa amekwenda siku ya kwanza wodini, lakini udhibiti huo kwa sasa umeshindikana kutokana na ndugu na jamaa na marafiki wanapokwenda kuwajulia hali, huweka dawa hiyo kwenye maji ya kunywa au kwenye juisi.

Binti amuua mama yake kisa kumnyang’anya simu yake

“Naomba viongozi wa maeneo yote washiriki kukemea matumizi ya dawa hizi zinazotumiwa kuharakisha uchungu kwa mjamzito kwa sababu zimekuwa ni moja ya sababu ya vifo kwa akina mama wajawazito katika mkoa wetu,” amesema.

Aidha, amesema vifo vitokanavyo na uzazi vinaendelea kupungua mkoani humo ambapo kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 kiwango cha vifo kilikuwa ni vifo 114 kwa vizazi hai 100,000 na kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Julai mwaka huu kiwango cha vifo kilikuwa vifo 96 kwa vizazi hai 100,000.

Send this to a friend