Jela miaka 100 kwa kukutwa na meno ya tembo

0
42

Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imewahukumu watu watano kifungo cha miaka 100 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano likiwemo la kukutwa na meno saba ya Tembo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Tumsifu Barnabas ambaye ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa Jamhuri katika shauri hilo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Barnabas amewataja waliohukumiwa kifungo hicho kuwa ni Mkazi wa Ushirombo mkoani Geita, Samson Emmanuel (48); Mkazi wa Itigi mkoani Singida, Shalali Jisandu (40); Mohammed Nasibu (32), mkazi wa Doroto; Mathayo Robert (48) na Hamis Ngurumo (52).

Miongoni mwa makosa waliyokutwa nayo ni kukutwa na silaha ya kivita aina ya G3 ambapo kila kosa limebeba kifungo cha miaka 20 jela.

Send this to a friend