Watanzania 22,000 walifariki kwa UKIMWI 2023

0
13

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kwa mwaka 2023 kufikia vifo 22,000, ikilinganishwa na vifo 29,000 vilivyotokea mwaka 2022.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani Dar es Salaam ambapo amesema idadi ya watu waliopima Virusi vya UKIMWI kwa mwaka 2023 imeongezeka tofauti na mwaka 2022.

“Idadi ya watu waliopima Virusi vya UKIMWI kwa mwaka 2023 ilifikia milioni 8.1 kutoka milioni 6.9 mwaka 2022. Pamoja na kwamba waliopima Virusi vya UKIMWI kwa mwaka 2023 walikuwa wengi, habari njema ni kwamba waliogundulika [kupata maambukizi] walikuwa wachache,” amesema.

Kwanini watu wengi wanapata maumivu ya kichwa mara kwa mara?

Waziri ameongeza kuwa idadi ya Watanzania milioni 1.663 wanaotumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI walipatiwa huduma ya dawa, ikilinganishwa na Watanzania milioni 1.612 waliopatiwa huduma hiyo mwaka 2022.

Aidha, amebainisha kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria mwaka 2023 vimepungua kufikia vifo 1,540 kutoka vifo 1,733 mwaka 2022.

Send this to a friend