DCEA yapongezwa ukamataji wa dawa za kulevya

0
28

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kufuatia ukamataji wa dawa za kulevya zaidi ya tani 3 na kueleza kuwa kukamatwa kwa dawa hizo ni ushindi mkubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Akizungumza na maafisa wa DCEA, katika makao makuu ya jijini Dar es Salaam Waziri Majaliwa ameeleza kuwa serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na mamlaka hiyo katika kupambana na dawa za kulevya.

Watanzania 22,000 walifariki kwa UKIMWI 2023

“Mafanikio haya yanaanza kuleta sura ya kwamba Tanzania si mahali sahihi kwa kuzalisha, kusafirisha, kuuza na sio mahali pazuri kwa matumizi ya dawa za kulevya,” amesema Majaliwa.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amemshukuru Waziri Majaliwa na serikali kwa ujumla kwa kuendelea kuiwezesha mamlaka hiyo kufanikisha kazi zake.

Dawa hizo zaidi ya tani 3 zilikamatwa Desemba 2023 katika eneo la Kibada, Dar es Salaam, ikiwa ni heroin na methamphetamine, ikiwa ni kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kukamatwa nchini tangu shughuli za udhibiti zianze kufanyika.

Send this to a friend