Kenya: Watakaobainika kuwa na vyeti feki watarudisha mishahara yote waliyolipwa

0
14

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini Kenya (EACC) imetoa onyo kuhusu matumizi ya vyeti feki vya masomo yanayofanywa na baadhi ya wananchi ili kupata ajira.

Akizungumza Mjini Kisumu Mwenyekiti wa EACC, Askofu David Oginde amesema suala la vyeti feki linazorotesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu.

Aidha, amesema Wakenya wanaopata ajira kwa kutumia vyeti feki watalazimika kurudisha mshahara wa kila mwezi, mali, na rasilimali walizopata kipindi walichofanya kazi.

“Tutalazimika kurudisha pesa zote ulizopata kupitia njia hiyo, hata kama umefanya kazi kwa miaka 20, tutataka pesa zote ulizopata wakati huo,” amesema Askofu Oginde.

Send this to a friend