Zanzibar yapiga marufuku wamasai kutembea na silaha

0
47

Serikali ya Zanzibar imepiga marufuku wamasi kutembea na silaha za jadi mitaani kwa kile ilchosema kuwa ni kuhatarisha maisha ya watu na ni kinyume cha utamaduni visiwani humo.

Katazo hilo limekuja baada ya video iliyosambaa mtandaoni ikiwaonesha wananchi wa jamii ya Kimasai wakimshambulia mfanyakazi wa halmashauri kwa silaha za jadi walipokuwa wakiendesha operesheni ya kusimamia sheria ndogo ndogo zinazozuia kufanya biashara maeneo ya barabara ya Mji Mkongwe.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi, Rashid Msaraka amesema utamaduni wa Zanibar hauruhusu watu kutembea na silaha za jadi mitaani, na kwamba baada ya kuzungumza na jamii hiyo wamekubali kuacha sime na marungu majumbani.

“Tumekubaliana kwamba kwakuwa utamaduni wa Zanzibar hauruhusu kutembea na silaha za jadi, hapa sio msituni hapa hakuna wanyama wakali, ni kufuata tu utamaduni wetu ulivyo, na wao wenyewe wamasai wamethibitisha kwamba unapokwenda kwenye tamaduni za watu zinaelekeza jambo fulani unapaswa kuzifuata, na wao wamekuwa tayari kuzifuata,” amesema.

Send this to a friend