TRC: Mgao wa umeme hautaathiri treni za SGR

0
41

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema mgao wa umeme unaoondelea nchini hautaathiri utendaji kazi wa treni ya abiria ya reli ya kisasa (SGR) kwani treni hiyo itakuwa na njia yake maalumu ambayo haifungamani na njia yoyote kwa ajili ya kusafirishia umeme.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa alipohudhuria jukwaa la lililolenga kuzungumzia umuhimu wa upatikanaji wa fedha endelevu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo amesema njia hiyo inawafanya kuwa na uhakika wa nishati hiyo.

“Sisi si watumiaji wakubwa wa umeme, watu wanadhani labda treni itatumia megawati 2,000 hapana, tuna imani kuwa umeme unaozalishwa na TANESCO na wanaotarajia kuingiza katika gridi utatosheleza sisi kuendesha treni,” ameeleza.

Ameongeza kuwa ikiwa umeme utakosekana nchi nzima na treni kushindwa kufanya kazi katika maeneo yao ya maunganisho ya treni (shunting) kuna vichwa vya treni vinavyotumia dizeli ‘hybrid’ ambavyo vinaweza kutumika kama mbadala.

Kadogosa amesema vichwa hivyo vipo vya aina tofauti ikiwemo vilivyowekwa betri ambayo ina uwezo wa kujichaji kadri treni inavyofanya kazi na baadaye nishati hiyo inaweza kutumika kwa dharura pindi kunapokuwa na tatizo.

Send this to a friend