Serikali imeiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuvunja mkataba na mkandarasi anayejenga jengo la abiria la kiwanja cha ndege cha Ruvuma kutokana na mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha jengo hilo kwa wakati.
Ameyasema hayo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile mara baada ya kutembelea na kukagua maboresho yaliyofanywa katika kiwanja cha ndege Songea.
“Serikali imewekeza bilioni 37 katika uwanja wa ndege huu, hivyo ni muhimu jengo la abiria likamilike kwa haraka. Nauelekeza uongozi wa TAA kuvunja mkataba na mkandarasi anayejenga jengo la abiria kwani ameshindwa kukamisha kwa wakati,” ameeleza.
Jengo hilo la abiria lilipaswa kukamika Juni 2023, lakini kufikia sasa lipo asilimia 30, ambapo ujenzi wake una thamani ya shilingi milioni 423.