Uingereza yapiga marufuku wafanyakazi wa afya wa kigeni kupeleka wategemezi

0
23

Serikali ya Uingereza imepiga marufuku wafanyakazi wa huduma za afya wa kigeni kuleta wanafamilia wanaowategemea nchini humo, hali inayopelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya wategemezi kuliko wafanyakazi wa huduma hizo.

Taarifa imeeleza kwamba, katika mwaka 2023, wafanyikazi 100,000 wa kigeni waliandamana kwenda Uingereza na jumla ya wategemezi 120,000.

Waziri wa Mambo ya Ndani, James Cleverly amesema kwamba wafanyakazi wa afya kutoka nje ya nchi wanachangia kwa kiasi kikubwa katika jamii hiyo, “lakini hatua hii inalenga kukabiliana na matumizi mabaya ya mfumo wa uhamiaji.”

“Sio sahihi wala haki kuruhusu hali hii isiyokubalika kuendelea. Tuliahidi watu wa Uingereza kuchuwa hatua, na hatutapumzika hadi tutakapotekeleza ahadi yetu ya kupunguza idadi kwa kiasi kikubwa,” amesema.

Kulingana na taarifa, mabadiliko hayo yataanza kutumika wakati serikali inajiandaa kuwasilisha sheria Bungeni mwishoni mwa wiki hii Machi 14.

Send this to a friend