Profesa Nyahongo: Miaka mitano ijayo wakazi wa Dar watatembea na oksijeni

0
28

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Julius Nyahongo ametoa tahadhari kuwa katika miaka mitano ijayo wakazi wa Dar es Salaam watalazimika kutembea na oksijeni kutokana na ongezeko kubwa la joto.

Akizungumza katika mdahalo wa kumbukizi wa miaka 102 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere amesema ongezeko hilo la joto linachangiwa na ukataji wa miti unaofanywa kiholela hali inayohatarisha mazingira.

“Makandarasi wanapotaka kujenga jengo wanafyeka eneo kubwa mno, wakiulizwa wanasema wanapima, wanasahau kuwa hiyo miti imehangaika sana kukua. Ninaomba Makamu wa Rais Dkt. Mpango waambie makandarasi wote wa Tanzania wanapotaka kujenga wakumbuke ile miti imeota pale kwa shida wakate sehemu ndogo wanayojenga pekee yake,” amesema.

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo, katika miaka ijayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watakosa oksijeni ya kuvuta na vibaka hawataiba simu, bali wataiba vitu vya kubeba oksijeni.

Profesa Nyamhongo amesema oksijeni inatengenezwa na miti na kwa sasa watu wa mijini wanataka wajenge kila sehemu pasipo kutenga eneo la kupanda miti jambo ambalo ni hatari kwa mazingira.

Send this to a friend