Lukuman Hemed, dereva wa basi la Shule ya Msingi Ghati Memorial lililosombwa na maji na kuua wanafunzi saba jijini Arusha amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka nane likiwamo la kuua bila kukusudia.
Ajali hiyo ilitokea Aprili, 2024 saa 12 afajiri baada ya gari hilo lililokuwa na watu 13 kutumbukia kwenye korongo na kusababisha wanafunzi hao kufariki baada ya kusombwa na maji.
Ajifungua mahakamani baada ya kuachiwa kwa tuhuma za mauaji
Dereva huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama, Sheila Mamento huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Aprili 30, mwaka huu baada ya mawakili wa upande wa Jamhuri kusema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Aidha, dhamana ya dereva huyo imepingwa na mawakili hao kwa madai ya kuwa usalama wake uko hatarini kutokana na wananchi kuwa na hasira na dereva huyo aliyesababisha ajali, japokuwa hakimu alitangaza dhamana kuwa wazi.
Hata hivyo, mshatakiwa huyo aliulizwa endapo anakubaliana na pingamizi hilo ambapo aliridhia na kupelekwa gereza la Kisongo hadi Aprili 30 mwaka huu.