Mbunge ataka Serikali irejeshe utaratibu wa pasipoti kuingia Zanzibar

0
34

Mbunge wa Jimbo la Konde, Zanzibar, Mohammed Issa amependekeza serikali irejeshe matumizi ya hati za kusafiria kwa ajili ya kuingia visiwani Zanzibar ikiwa ni pamoja na raia wa Tanzania Bara ili kuvilinda visiwa hivyo kwa kudhibiti wimbi la watu wanaoweza kusababisha uhaba wa makazi.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, amesisitiza kwamba Zanzibar ina eneo dogo la ardhi na hivyo ni lazima kulindwa.

Serikali ya Zanzibar yalaani unyanyasaji unaofanyika kwa sababu za kidini

“Sikubaliani na dhana ya kupuuza kuvilinda visiwa hivi, Zanzibar hivi sasa imejaa watu wengi, na tukiendelea hivi watu watakosa sehemu za kuishi. Nampongeza sana Karume kwa kujenga hayo majengo makubwa kwani alitaka kila mtu akae pale Zanzibar.

Kama ilivyo Zanzibar ni ndogo sana, bado naunga mkono kurejeshwa kwa pasipoti ili kuhakikisha ulinzi wa raia wanaoingia Zanzibar,” amesema.

Send this to a friend