Wanaodaiwa kusambaza picha za ngono WhatsApp wafikishwa mahakamani
Wanaume wawili, Furaha Jacob pamoja na Mustapha Kuhenga (28) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakituhumiwa kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.
Jacob ambaye ni mkemia na Kuhenga mtaalamu wa TEHAMA, wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.
Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi amesema shtaka la kwanza la shambulio la mtandao linamhusu Jacob pekee ambapo Februari 11, 2024 anadaiwa kutuma video WhatsApp yenye maudhui ya ngono kupitia simu yake kwa lengo la kumtishia Mihayo.
Kwa upande wa Kuhenga anadaiwa kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 alituma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu yake kupitia mtandao wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo Mihayo.
Polisi wakanusha kuhusika na kifo cha Babu G
Shtaka la mwisho linawahusu watuhumiwa wote wawili ambapo wanadaiwa kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp za Mihayo Desemba Mosi 2023 na Machi 2024.
Aidha, watuhumiwa wote wamekana mashtaka hayo na tayari wapo nje kwa dhamana ya shilingi milioni 3 huku kesi ikiahirishwa hadi Mei 9, mwaka huu.
Chanzo: Mwananchi