Vyuo Vikuu 10 bora zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara

0
66

Ripoti iliyotolewa na Times Higher Education imeorodhesha vyuo vikuu bora katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Orodha hiyo inalenga kuangazia taasisi za elimu ya juu barani Afrika pamoja na kushughulikia changamoto za elimu ya juu katika eneo hilo.

Kulingana na ripoti, orodha hiyo inaongozwa na Chuo Kikuu cha Witwatersrand kilichopo nchini Afrika Kusini, Chuo Kikuu cha Johannesburg kikishika nafasi ya pili huku Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kilichopo nchini Tanzania kikishika nafasi ya tatu.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa takriban theluthi mbili ya vyuo vikuu vinavyoshiriki ni taasisi za umma; robo ya vyuo hivyo ni mashirika binafsi, yasiyo ya faida; na karibu moja ya kumi ni mashirika binafsi, ya faida.

Hivi ni vyuo vikuu bora katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mujibu wa Times Higher Education;

  1. Chuo Kikuu cha Witwatersrand – Afrika Kusini
  2. Chuo Kikuu cha Johannesburg – Afrika Kusini
  3. Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – Tanzania
  4. Chuo Kikuu cha Pretoria – Afrika Kusini
  5. Chuo Kikuu cha Makerere – Uganda
  6. Chuo Kikuu cha Western Cape – Afrika Kusini
  7. Covenant University – Nigeria
  8. UGHE – Chuo Kikuu cha Usawa wa Afya Ulimwenguni – Rwanda
  9. Chuo Kikuu cha Ashesi – Ghana
  10. Chuo Kikuu Ardhi – Tanzania
Send this to a friend