Kushiriki kufanya mapenzi si tu shughuli ya kufurahisha kimwili, bali pia ina athari kubwa kiafya ambazo zinaweza kuwa na faida kubwa kwa mwili na akili.
Kutofanya mapenzi kwa muda mrefu kunaweza kuwa na athari mbalimbali, lakini athari hizi zinaweza kutofautiana kwa watu tofauti kulingana na sababu za kisaikolojia, kiafya, na kijamii.
Hapa kuna baadhi ya mambo yanayoweza kutokea unapokuwa hushiriki kufanya mapenzi kwa muda mrefu;
Msongo wa mawazo na wasiwasi
Baadhi ya watu wanaweza kuhisi msongo wa mawazo au huzuni kutokana na kutofanya mapenzi kwa muda mrefu, hasa kama ilikuwa chanzo cha furaha.
Kushiriki tendo hili hufanya mwili utoe homoni kama vile oksitosini na endorphins, ambazo zinaweza kusaidia kudhibiti athari za msongo wa mawazo.
Kumbukumbu
Utafiti bado uko katika hatua za awali, lakini baadhi ya tafiti zimeonyesha kwamba watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara wana uwezo mzuri katika kumbukumbu. Pia inaweza kusaidia ubongo kufanya kazi vizuri.
Saratani ya Prostate kwa wanaume
Kwa wanaume, kufanya mapenzi kunaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya prostate, ingawa kuna mambo mengine ya kuzingatia pia kama vile usalama wa ngono.
Utafiti fulani unasema wanaume ambao hufanya mapenzi chini ya mara moja kwa wiki wanaweza kuwa na uwezekano mara mbili zaidi wa kupata tatizo la dysfunction ya erectile (ED) ikilinganishwa na wale wanaoshiriki mara kwa mara.
Maumivu ya mgongo
Wataalam wanasema kufanya mapenzi kunasaidia kupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, na miguu na pia husaidia maumivu ya ugonjwa wa viungo na hedhi.
Wanaume na wanawake waliopoteza wenza wao, wanaweza kuwa na matatizo ya mgongo ya mara kwa mara kwa sababu ya kutoshiriki tendo la ndoa.
Uwezekano wa matatizo ya kijinsia baadaye
Kutokushiriki kufanya mapenzi kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo kama vile kupoteza hamu ya tendo la ndoa hapo baadaye au maumivu wakati wa kushiriki tendo kwa wanawake.
Kupoteza umakini katika kazi
Utafiti unaonesha kuwa, mwanaume au mwanamke anapokaa muda mrefu pasipo kufanya mapenzi, uwezo wa kufanya kazi katika ufanisi unaotakiwa na ubunifu unaweza kupungua.