Asilimia 4 ya watoto nchini wanafanyiwa ukatili mitandaoni

0
26

Matokeo ya utafiti wa kujua kiwango cha ukatili dhidi ya watoto kupitia mitandao (online child abuse) wa mwaka 2022, umebainisha asilimia 67 ya watoto wa umri wa miaka 12 hadi 17 wanatumia mitandao ambapo, kati yao asilimia 4 wamefanyiwa vitendo vya ukatili na uonevu mitandaoni.

Hayo yameelezwa katika bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum iliyosomwa bungeni na Waziri Dkt. Dorothy Gwajima kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2024/25.

Bajeti hiyo imeeleza kuwa katika jitihada za kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mitandaoni, wizara imezindua Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni kuelimisha watoto, wazazi, walezi, walimu, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zisizo za serikali, wizara za kisekta, na jamii kuhusu kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili mitandaoni na maeneo mengine.

Imebainisha kuwa matumizi ya mitandao hayawezi kuepukwa kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo mitandao ni sehemu ya maisha hasa kwa kizazi kilichopo sasa.

Send this to a friend