Maisha ni safari yenye changamoto na furaha, yenye mabadiliko na maendeleo. Unapaswa kuyafurahia maisha kwa kufanya kile kilicho sahihi pasipo kujali nani anasema nini.
Haya ni mambo muhimu ambayo watu huchelewa kujifunza maishani mwao;
1.Muda
Maisha ni mafupi na kila mtu atakufa. Kilicho muhimu ni kufurahia maisha, kupenda na kufanyia watu wema.
2. Kuacha Kulalamika
Wengi hupoteza muda kulalamika juu ya matatizo madogo madogo. Hivyo muhimu ni kufanya majukumu yako ipasavyo pasipo malalamiko na kuwa na mawazo chanya.
3. Hofu
Hofu ni hisia ya kawaida lakini haileti mafanikio. Wengi hushindwa kufanya mambo sahihi kutokana na hofu zao, hivyo jaribu kufanya kile kinachokupa hofu zaidi na pengine ikaleta matokeo usiyoyatarajia.
4. Familia
Urafiki na mahusiano ni muhimu, unapaswa kujenga familia ukiwa bado na nguvu na kutengeneza marafiki waaminifu ambao unaweza kuwategemea.
5. Usijaribu kumbadilisha mtu
Talaka nyingi hutokea kwa sababu ya matarajio yasiyo halisi. Watu hudhani wanaweza kubadilisha wenza wao, lakini hapo baadaye wanagundua hawawezi.
6. Kujipenda
Wewe ni wa kipekee. Ni muhimu kuishi maisha bora na kujipenda, kujijali, na kujiheshimu.
7. Usipuuze maisha
Watu wengi wana majukumu, na ratiba za kila siku ambazo zinachosha sana. Lakini usipoteze muda kwa kazi ambayo haikupi furaha au faida.
8. Kujali nini watu wanafikiri
Usipoteze maisha yako ukijali wengine wanavyokufikiria. Wengi wanajali maisha yao wenyewe.
9. Kuongeza maarifa
Unapaswa kutambua kwamba, watu wenye kuvutia maishani ni wale wenye udadisi na wanaotafuta maarifa. Watu wasio na uelewa wanaweza kuwa na ujinga na wenye kuudhi wakati mwingine.
10. Hifadhi pesa
Watu wengi hutumia pesa zao pasipo kuhifadhi kiasi kwa ajili ya kuwasaidia katika wakati ujao. Lakini pia hujui siku ya dharura inaweza kuja lini. Hivyo anza kuhifadhi pesa.
11. Furaha
Furaha mara nyingi ni uamuzi wa mtu. Usitafute kitu au mtu wa kukuletea furaha, bali unapaswa kuitengeneza wewe mwenyewe.
12. Afya
Jali afya yako ikiwa bado unaweza. Kula vizuri, kunywa maji mengi, na ufanye mazoezi ili hapo baadaye usitumie pesa zako ulizotengeneza kwa muda mrefu kufanya matibabu.
13. Kuwa wewe mwenyewe
Watu wengi wanaruhusu hofu na aibu kuwazuia kuwa wao wenyewe na kufanya mambo wanayoyataka. Usiruhusu chochote kikuzuie kuwa wewe mwenyewe.
14. Umri ni namba tu
Huwezi kuwa mzee sana kujaribu kitu kipya, na usiruhusu mtu yeyote akwambie vinginevyo. Jitunze, na fuata ndoto zako.
15. Kusamehe
Ruhusu kusamehe watu waliokukosea au kujisamehe wewe mwenyewe na kuachilia vitu. Hii itakupa amani ya moyo na akili pia.
16. Kila mtu anapitia magumu
Usidhani ni wewe pekee unayepitia magumu, huwezi kujua mawazo yaliyo ndani ya mtu. Mtu anaweza kuonekana kuwa na maisha mazuri, lakini ukweli unaweza kuwa tofauti kabisa.
17. Kusafiri
Kila mtu ana ratiba na bajeti tofauti. Licha ya hali yako, jaribu kuchukua fursa yoyote unayoipata kutembea duniani na kujifurahisha. Hii itakusaidia kupata uzoefu wa tamaduni mbalimbali.
18. Kuwa mkweli
Kusema ukweli kunaweza kuonekana kuwa ngumu zaidi kuliko kusema uongo wakati mwingine, lakini kusimama kwenye ukweli ni chaguo bora zaidi kwa ajili ya amani yako ya ndani