Wanaotuhumiwa kuvunja na kuiba usiku wakamatwa Rukwa

0
91

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limesema katika kipindi cha mwezi Julai, 2024 limekamata watuhumiwa 28 wakijihusisha na matukio ya uvunjaji hasa nyakati za usiku.

Katika taarifa iliyotolewa kwa umma na Jeshi la Polisi imesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na mali zidhaniwazo kuwa za wizi ambazo ni vitenge doti 46, simu janja 1, redio 4, runinga 7 zenye ukubwa tofauti tofauti, kompyuta mpakato 1, kishikwambi 1 na trei ya vyombo 1.

Aidha, Jeshi la Polisi limewakamata watu wanne wakiwa na nyara za Serikali ambazo ni meno ya tembo, miguu mitano ya mnyama insha, magamba 20 ya mnyama kakakuona na nyama ya nguruwe pori.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu hasa kujichukulia sheria mkononi na kutoficha taarifa za uhalifu .

Send this to a friend