Polisi: Uchunguzi wa binti aliyefanyiwa ukatili unaendelea vizuri

0
111

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa wa video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha tukio la binti aliyefanyiwa vitendo vya ukatili unaendelea vizuri hivyo wananchi waendelee kuwa na subira kwani taarifa itatolewa baada ya kukamilisha yale ambayo sheria za nchi zinavyoelekeza.

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema limekuwa likipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kujua uchunguzi umefikia hatua gani.

“ Tunaendelea kusisitiza mwenye taarifa ya ziada atuwasilishie kwa njia iliyo sahihi kwa kutumia mifumo iliyopo bila kuendelea kumuumiza,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, Jeshi hilo limetoa wito kwa Watanzania kutafakari namna wanavyoendelea kujadili tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kwani inaweza kuwa inawatonesha majeraha familia na muathirika wa tukio hilo.

Send this to a friend