Rais aelekeza viwanda vilivyokufa Morogoro vifufuliwe

0
58

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itahakikisha Mkoa wa Morogoro unarudi kwenye hadhi ya viwanda kama ilivyokuwa hapo zamani ili kukuza uchumi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza leo na wananchi wa Mkoa huo katika Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, Rais Samia amesema Serikali itahakikisha inalinda viwanda vya Mkoa wa Morogoro visife huku akiagiza viwanda vilivyokufa vifufuliwe.

“Tunataka kurudisha hadhi ya Morogoro ya viwanda, na tunaka Morogoro ikashindane na Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Tayari Waziri wangu wa viwanda nimeshamuelekeza kuhakikisha viwanda vilivyopo havifi, lakini vile vilivyokufa basi vifufuliwe hata kama havitazalisha yale mazao yaliyokuwa yakizalishwa, lakini viwanda vile vifufuliwe vizalishe mambo mengine viendelee na kazi.

Aidha, Rais Samia amesema ombi lililotolewa la kuupandisha hadhi mkoa huo kuwa jiji, kwasasa bado haujafikia viwango vilivyowekwa hivyo jitihada kubwa bado inahitajika ili kufikia viwango hivyo.

Mbali na hayo amewatoa hofu wakazi wa Morogoro kuhusu upatikanaji wa maji akieleza kuwa ifikapo mwaka 2025 serikali itakuwa imekamilisha miradi ya maji nchini kama ambavyo ilani inavyoelekeza.

Send this to a friend