Masoud Kipanya amfungulia rasmi mashtaka Mwijaku akidai fidia kwa kumchafua

0
95

Mchoraji wa katuni maarufu na mtangazaji, Ally Masoud maarufu kama Masoud Kipanya amemfungulia mashtaka Burton Mwemba ‘Mwijaku’ kwa tuhuma za kumchafua kwenye mitandao ya kijamii.

Mahtaka hayo yaliyofunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania Agosti 05, 2024 yanamtuhumu Mwijaku kumkashifu kwa maandishi Juni 04 kupitia ukurasa wake wa Facebook na Insta yakiwa yenye maneno ya kumfedhehesha ikiwemo kujihusisha na biashara haramu, ka

Masoud amesema maneno hayo yamemuathiri kiajira, kibiashara, kimahusiano ndani ya jamii ya Kitanzania kuanzia kwenye familia yake, kisaikolojia na kumshushia heshima na hadhi aliyoijenga kwa jasho na damu kwa zaidi ya miaka 35.

Kutokana na kashfa hiyo, Masoud ameiomba mahakama imuamuru Mwijaku amlipe fidia ya madhara halisia atakayothibitisha kwa ushahidi mahakamani kutrokana na kashfa hiyo ya TZS milioni milioni 500 na fidia ya madhara ya jumla yatakayopimwa na kuridhiwa na mahakama kwa mamlaka yake ya TZS bilioni tano.

Aidha, Kipanya ameiomba mahakama itamke katika hukumu yake kwamba maneno aliyotamka hayana ukweli yenye nia ya ovu na kuharibu hadhi na heshima yake na pia mahakama iamuru Mwijaku kuomba radhi bila masharti na kuondoa mitandaoni maneno ya kashfa yaliyoandikwa na kusambazwa.

Hata hivyo, nyaraka zilizotolewa kupitia mawakili wake, imesema tayari mlalamikiwa amekwishapelekewa wito wa kuitwa mahakamani na kutakiwa kuwasilisha maelezo ya utetezi ndani ya siku 21 tangu alipopokea wito huo.

Chanzo: Jamii Forums

Send this to a friend